GET /api/v0.1/hansard/entries/1480921/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1480921,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1480921/?format=api",
"text_counter": 154,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, wale wanaosimamia uchaguzi lazima sheria iwaangazie. Kukiwa na ukiukaji wa sheria wakati wa uchaguzi, ni muhimu wanaohusika wapelekwe mahakamani na kushtakiwa kwa makosa hayo. Haiwezekani msimamizi wa uchaguzi akatae kuhesabu kura halali iliyopigwa na mwananchi wa Kenya. Haiwezekani msimamizi wa uchaguzi kutangaza mtu aliyeshindwa kuwa mshindi bila kuchukuliwa hatua yoyote kwa mujibu wa sheria. Kwa hivyo, sheria hii itasaidia kuwachukulia hatua watakaopeleka matokeo yasiyo sawa wakati wa uchaguzi nchini Kenya. Kwa hayo maswala mawili, naunga mkono marekebisho ya Sheria ya Makosa ya Uchaguzi."
}