GET /api/v0.1/hansard/entries/1480995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1480995,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1480995/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(IEBC) ipewe fedha ili iweke mitambo na teknolojia inayotakikana katika vituo hivi. Mara kwa mara, tumeona matatizo kama vile ukosefu wa umeme na vifaa vya kuhifadhia makaratasi ya kupiga kura katika vituo kadha wa kadha vya upigaji kura. Wakati mwingine, mvua ikinyesha magari ya kusafirisha masandaku ya kura yanakosekana. Hivyo basi, naunga mkono mchakato wa marekebisho ya sheria za uchaguzi. Vile vile, naunga mkono marekebisho ya sheria ya kuondoa kiwango cha masomo ya cheti cha shahada kwa wagombeaji uchaguzi kwa nyadhifa ya Members of the County Assembly (MCAs), Seneta, Women Representatives na Members of Parliament (MPs). Hatusemi elimu ni mbaya. Tunajua ya kwamba elimu bora ni msingi wa maisha wa vijana wetu. Lakini, tumeona wafanyibiashara wengi wakarimu wakisaidia watu mashinani. Japo haiwezekani, ningetamani sana pia kama kigezo cha gavana kuwa na elimu ya shahada kingeondolewa. Wapo watu wengi wanao ujuzi na hekima kama Mfalme Sulemani wa Biblia. Vile vile, naunga mkono pia mapendekezo ya kuwalipa wafanyikazi wa muda wanaoajiriwa kufanikisha uchaguzi kama vile madereva. Wengi wao mpaka sasa hawajalipwa. Hili ni jambo la aibu sana. Changamoto kubwa imekuwa katika mchakato wa kutoa kandarasi ya kutoa huduma hizi. Marekebisho haya yatuzuia mambo mengi kwenda mrama. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}