GET /api/v0.1/hansard/entries/1481050/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1481050,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1481050/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Namkaribisha Waziri wetu mkuu kwa Bunge letu la Seneti. Swali langu linahusu nambari ya watu wanaofanya kazi katika Ubalozi wa Kenya huko Marekani. Awali nilikuwa nafanya kazi katika Wizara inayohusika na nchi za kigeni. Kulikuwa na shida kubwa pale kwa sababu watu wengi hutamani kutoka Kenya ili wafanye kazi katika nchi za nje. Ubalozi wa Amerika umeahidi kwamba pesa zikipatikana utaongeza nambari ya wafanyikazi kule. Tunataka kujua katika harakati za kugawa zile nafasi, ni watu wangapi watatoka Kaunti ya Tana River na zinginezo? Tunataka usawa. Hatutaki Wizara iwe na ubaguzi wa kuchukua watu kutoka pande fulani. Ni watu wangapi watatoka katika Kaunti ya Tana River? Na ijapokuwa hawapo basi, katika ile breakdown ya wanaofanya kazi kule kuna usawa? Iwapo hakuna usawa, una mipango gani ya kuhakikisha kuwa katika ubalozi wa Kenya huko Marekani pamoja na zingine, kuna usawa kwa wanaoenda kufanya kazi?"
}