GET /api/v0.1/hansard/entries/1481187/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1481187,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1481187/?format=api",
"text_counter": 183,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Mimi ninasumbuka kwa sababu, tayari tumejitia kitanzi kwa kutenga siku za kujadili Hoja hii. Vile vile tutakapokuwa katika Hoja ile halafu kuweko na masuala mengine nyeti, tutajipata katika ile sehemu ya kwamba, hatuna muda wa kutosha kuyaangazia masuala yale kiundani. Hatuwezi kuendelea siku ile nyingine ambayo ni Jumatano kwa sababu tayari tumeitenga kwa shughuli nyingine tofauti.Kwa hivyo kuendelea mbele, pengine tuwe tukipea muda zaidi. Hata hivyo, ninaunga mkono."
}