GET /api/v0.1/hansard/entries/1482338/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1482338,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1482338/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "watoto wetu ndio hufagia. Pale juu ya gari, alisema Gavana atoe pesa za mafuriko, wakati alijua Ksh14 bilioni kutoka World Bank ambazo ni za Disaster Management zilikuwa kwa ofisi yake na aliziramba. Alikuwa anajua tuliweka Kshs6 bilioni kwa bajeti na hakuzileta Mombasa. Yule ni kiongozi wa kugonganisha watu. Ndio maana najiuliza kwa miaka miwili, ana kampuni 22. Mimi sina hata moja. Miaka miwili na ana kampuni 22 na zote zina Kshs5.7 bilioni ya mtoto na mke, na kisha bado anaenda kuchukua mali ya ndugu yake. Unawacha mayatima na unatesa mjane. Kisha, utatuambia nini katika taifa la Kenya?"
}