GET /api/v0.1/hansard/entries/1482440/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1482440,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1482440/?format=api",
    "text_counter": 282,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi South, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
    "speaker": null,
    "content": "Kisa na sababu ni uwongo ambao Naibu Rais ameujaza katika matamshi yake. Jana jioni, nilichukua muda wangu kumsikiliza kwa hoja aliyokuwa anaizungumzia. Nashukuru kwa kunipa nafasi hii, kwa sababu mimi ni mmoja kati ya wale walioguswa. Kama Mbunge wa Eneo Bunge la Kilifi Kusini, ile hoteli ya Gachagua imejengwa katika eneo bunge langu. Yale aliyoyazungumza Bwana Deputy President jana ni uwongo mtupu. Kitu cha kwanza, wakati King Charles III alipokuja ndio aende atembelee kule chini Kuruwitu, alikuwa amekuja kwa mwaliko wa Kuruwitu Conservation and Welfare CommunityBased Organisation (CBO). Alipofika Kuruwitu Conservation and Welfare CBO, ule mkutano haukuchukua zaidi ya dakika thelathini, halafu akaenda Vipingo Ridge. Ile barabara ambayo aliomba itengenezwe kwa sababu angetaka kuhifadhi ile Kuruwitu Conservancy haipitiki. Lakini Deputy President akaona amepata nafasi nzuri sana ili ile barabara, badala iende Kuruwitu Conservancy, akaichukua akaijenga akiipeleka kwake hotelini. Imeishia pale kwa hoteli yake. Naongea kwa sababu mimi pia nimejenga papo hapo. Bwana Deputy President alisema kuwa watu waliomba hiyo barabara ijengwe, na kulikuwa na public participation . Ni kweli kabisa tuliomba ile barabara ijengwe, lakini hii kwamba ni uhusiano wake na wenyeji wa Kuruwitu ambao ni mzuri na wanaelewana, na kwamba ata Mbunge wa eneo hilo anajua, nasema ashindwe katika jina la Yesu! Siyajui hayo. Sikuhusishwa kuhusu barabara ambayo amepeleka kwa hoteli yake."
}