GET /api/v0.1/hansard/entries/1482565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1482565,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1482565/?format=api",
"text_counter": 407,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante, Mhe. Spika. Umoja wa taifa ni muhimu sana. Naibu wa Rais haleti umoja. Nataka ieleweke kwamba watu wa mlima wanaishi sehemu zingine. Kule kwangu, Kiunga, niko na watu wa mlima. Kile wanachoona zaidi ni sanddunes . Hawaoni mlima. Wanaona bahari. Naibu wa Rais alizungumzia kuhusu National Intelligence Service (NIS) ambayo ilikuwa grave mistake . Alikosea sana. Afadhali angetaja Noordin kama ako na shida naye kuliko taasisi ya Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa. Inatufanya tukae dhaifu mbele ya maadui zetu. Kwa mfano, Al-Shabaab watatuona vipi kama tuko wadhaifu? Kwa mtu yeyote, haswa mwanaume anayetukana mwanamke, kila mtu aliyeumbwa ana shimo saba. Wanaume na wanawake wanazo. Kama ni malaya, basi ni wote. Nimechoka kusikia hili jina. Naulizwa kama mashimo ni haya mawili ya pua, masikio, mdomo na yale mengine mawili ambayo kila mtu anayo. Kwa Kiislamu, tunafundishwa kuheshimu wajane na mayatima. Dini yetu hairuhusu mtu ambaye hawaheshimu. Asante, Mhe. Spika."
}