GET /api/v0.1/hansard/entries/1482973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1482973,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1482973/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohamed",
    "speaker": null,
    "content": "Government Affirmative Action Fund (NGAAF) ya kujenga sehemu ambayo ni Gender Based Violence Centre. Sasa yaelekea mwaka wa tatu kutoka approval ya ile project . Shida ni kuwa barabara ambayo inahusu county government haijajengwa. Mpaka juzi, nimemuomba Mbunge wa Kisauni, Mhe. Rashid Bedzimba, na nataka nimpongeze hapa, kwa sababu yeye ndiye alinichimbia barabara. Afadhali hizi pesa za KeRRA zipatiwe Wabunge. Gavana huwa hawatumii peza zao kutengeneza barabara. Tunaweza kuwashika mkono hawa Wabunge, angalau watujengee barabara. Ni aibu sana kuona Mbunge akiomba na kuandika mabarua hadi anachoka. Mheshimiwa anafanya public participation lakini hana pesa za kujenga barabara mpaka sehemu ambayo akina mama waliodhulumiwa, wanaweza kupata usaidizi. Imekuwa ngumu mpaka Bedzimba akaomba tractor ili anipitishie kando kidogo ndio nipate mahali pa kujenga. Nataka kuwapongeza Wabunge wa Mombasa. Ukienda kwa ndugu yangu Bady, kuna barabara safi na nzuri sana. Lakini ukiangalia za kaunti, ni kama blanketi zimetoka hapa hadi pale; yani ziko mita 100. Hatuelewi hizi pesa zinafanya nini. Zipatiwe hawa Wabunge. Najua wengine wetu tunatamani kuwa magavana lakini hizo pesa ziingie kwa mikono ya Wabunge. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}