GET /api/v0.1/hansard/entries/1483090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1483090,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483090/?format=api",
    "text_counter": 254,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kitui South, JP",
    "speaker_title": "Mhe. (Dkt) Rachael Nyamai",
    "speaker": {
        "id": 13374,
        "legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
        "slug": "richard-ken-chonga-kiti"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nakushukuru sana kwa kunipatia fursa hii niwakaribishe wanafunzi kutoka shule ya Muthwani. Ningependa kuwakaribisha sana katika Bunge hili. Hapa ndipo tunapotunga sheria za nchi ya Kenya. Tunahakikisha kwamba Serikali kuu na serikali za kaunti zinapata fedha za kufanya maendeleo. Vile vile, tunafuatilia jinsi pesa ambazo tumewapatia zinatumiwa. Kwa hivyo, bila kupoteza wakati, ninawashukuru sana. Ningependa kujiunga na wewe, kama Naibu Spika aliye kwa Kiti sasa hivi, pamoja na Wabunge na Spika wetu, Hon. (Dr) Moses Masika Wetangula, kuwakaribisha wanafunzi na kuwaambia wasome kwa bidi kwa sababu wao ndio viongozi wa kesho."
}