GET /api/v0.1/hansard/entries/1483186/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1483186,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483186/?format=api",
    "text_counter": 350,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi nichangie Mswada huu kuhusu Maktaba ya Kitaifa. Mwanzo, ninaipongeza Kamati kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mhe. Wanyama. Wamefanya jambo la maana kwa sababu sheria hii ilikuwepo kabla ya ugatuzi. Hivyo, kulikuwa na haja kubwa ya kuweka hii sheria baada ya mwaka wa 2010 kuhusu mambo ya ugatuzi. Kwa hivyo, ilikuwa muhimu sana afanye hivyo. Sheria inasema kuwa, kuna haja ya kuwa na maktaba angalau katika makao makuu ya kaunti, lakini kuna kaunti zingine kama Lamu ambazo hazina maktaba hata moja. Hii sheria ikitungwa, ningependa Kamati izingatie kuwa kaunti zingine ambazo hazina maktaba hata moja zisiachwe nyuma. Ugatuzi ulipokuja, hapakuwa na maktaba kwenye Kaunti ya Lamu. Kwa hivyo, kuna kaunti nyingi kama hiyo ambazo hazina maktaba. Kwa hivyo, sheria kama hii ikitungwa, kule kwetu tunajiuliza: Inatungiwa nani? Pia, ningependa kujuza Kamati kwamba wenzangu walivyosema, nami pia narudia kuwa teknolojia imesonga sana. Kuna ICThubs ambazo Rais alisema zijengwe katika kila wadi. Kwa nini tusichukue hii nafasi kubadili sheria hii iseme kuwa, kwenye kila wadi kujengwe maktaba ambayo itatumia teknologia? Itakuwa rahisi kuliko kwenda kujenga kwa kila wadi, eneo bunge au kaunti. Tunaweza kutumia raslimali zilizopo tuwe na maktaba ili watu wapate kusoma. Kama tulivyoambiwa na Wabunge wenzangu, siku hizi watu wanahamia kwenye mambo ya dijitali. Pia, hapo nyuma tulikosa. Kuanzia saa hii kwenda mbele, tutazungumzia kwenda kwenye upande wa hiyo teknolojia lakini kukosekana kwa maktaba kunaregesha eneo nyuma sana. Kwa mfano, sisi kwetu Lamu, Kaunti nzima hatuna maktaba. Imesababisha watu kuandika vitu visivyo vya ukweli. Kuna mambo mengi ya kihistoria. Kwa mfano, kule Shanga kuna msikiti yenye kibla mbili. Kibla moja ikielekea Masjid Aqsa. Hiyo ni historia kubwa inayomaanisha karne na karne. Ilhali katika historia, hakuna vitu kama hivyo. Saa zingine watu hutuuliza: “Nyinyi kwenu si Kenya. Kwa hivyo, asili yenu ni ipi?” Inamaanisha Uislamu ulikuwepo kabla Kenya iwe tayari. Kijiji kinaonyesha kuwa wakati wa kuswali, Waislamu walikuwa wanaelekea Al-Aqsa kabla waanze kuelekea Mecca. Kwa hivyo, kukosekana kwa hizo maktaba ndiko kunakosababisha kukosekana kwa hizo kumbukumbu. Zingekuwepo kumbukumbu, tungejua tunakotoka. Sasa hivi, wengine tukiamua kufanya DNA, sijui itajulikana tuna asili ipi ila huenda sisi tukawa wenye asili ya Kikenya zaidi kushinda wengine. Ni karne nyingi tangu wazazi wetu watoke pale walipokuwa. Kulikuwa na haja sana lakini pia kwa sasa, serikali ya kaunti na ile ya Kitaifa yaweza kutekeleza hilo jukumu. Tunataka kujua historia kwa sababu inashangaza kuwa hayo mambo hayaaminiki. Siyo kabila zote zikioana kunatokea kabila nyingine ijapokuwa inasemekana kwenye historia ya Mbajuni kwamba ni Mmijikenda na Mwarabu walioana ndipo akazaliwa Mbajuni. Na ambapo utaona Mkikuyu akioana na Mkamba, haizaliwi kabila nyingine. Isipokuwa wakati Mmijikenda alipoolewa na Mwarabu, ndio ikapatikana Mbajuni. Inashangaza! Hizi historia lazima zijulikane. Kama zimejulikana, zingekuwa kwenye hifadhi za maktaba zetu ambapo ingekuwa rahisi kujua mambo kama hayo. Kaunti ina jukumu lakini national Government inatakikana isukume, hata kama ni upande wa kuweka policy . Hii Kamati ina kazi ngumu zaidi kwa vile imesema hii Bill ni ya Kamati ya Michezo na Makavazi. Nataka waangalie mambo ya maktaba na makavazi ambayo yako Kenya yetu ambayo ni vivutio vya utalii ili watu wafaidike. Kule Lamu kuna makavazi mengi na sheria nyingi ambazo zimewekwa na zinamkandamiza mwananchi anayeishi pale. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}