GET /api/v0.1/hansard/entries/1483261/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1483261,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483261/?format=api",
    "text_counter": 23,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Ninakushukuru kwa kusikiilza ombi la Kiongozi wa Seneti wa Walio Wengi, Sen. Cheruiyot, na kuruhusu Wawakilishi wa Wadi kusikiliza kesi hii. Mimi pia nilikuwa Mwakilishi wa Wadi na ni vizuri kuhudhuria kikao kama hiki na kushuhudia kwa sababu kesho wataweza kuwa hapa pia. Katika Kanuni zetu za Kudumu, Nyongeza ya Tatu ambayo inatoa masharti ya utaratibu wa kusikiliza na kuamua mashtaka ya kumwondoa gavana mamlakani; Kanuni ya Kudumu namba 80(12) inasema masharti ambayo yamepeanwa yakizingatiwa, gavana atasikilizwa na ushahidi utakapoanza, utaendelea hadi Seneti itakapohitimisha kusikiliza swala hilo. Bw. Spika, tumeanza kusikiliza jambo hili na Kanuni zetu za Kudumu zinasema kuwa tunapoanza, tunafaa kuenda mpaka mwisho. Seneti kwa sasa, haiwezi kuangalia namba ilikuwa namna gani. Tutaangalia makosa ambayo yataletwa hapa na tutasikiliza pande zote mbili na mwishowe tutaamua kesi baada ya kusikiliza kila kitu. Bw. Spika, mahali ambapo utatuelekeza, ni vizuri Maseneta wapewe nafasi kuamua jambo hilo. Hii ni kwa sababu kulingana na vile nimesikiliza kesi kutoka kwa wakili wa gavana wanakualika kufanya uamuzi. Sidhani kwamba uamuzi unaweza kufanywa na Spika peke yake katika muda huu. Lakini Maseneta wote wanafaa wasikilize kesi halafu waweze kuamua."
}