GET /api/v0.1/hansard/entries/1483716/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1483716,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483716/?format=api",
"text_counter": 74,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii kuiunga mkono Ripoti ya Kamati ya Fedha na Bajeti ya Bunge hili kuhusiana na sheria ya County Governments Additional Allocations Bill (Senate Bills No.19 of 2024). Kamati iliangalia marekebisho iliyokuwa imependekezwa na Bunge la Kitaifa kuhusiana na Mswada huu wa sheria. Tuliona kwamba Bunge la Kitaifa lilifanya makosa kuhusiana na maswala hayo. Kwanza, walipunguza fedha zinazotoka katika Serikali ya kitaifa kuja katika serikali za kaunti. La pili ni kuwa hata zile fedha ambazo wanakusanya kwa niaba ya kaunti zetu zimepunguzwa, kwa mfano, faini zinazolipwa kwa makosa inayohusiana na sheria za kaunti ambazo zinakusanywa na mahakama. Fedha hizi zinastahili kuenda katika mfuko wa serikali zetu za kaunti, zile ziko na mahakama. Kwa mfano, Kaunti za Mombasa na Nairobi ambazo ziko na mahakama ambayo husimamia mashtaka yanayofanyika kuhusiana na sheria za kaunti. Kwa mfano, mtu kujenga nyumba bila kibali cha kaunti au wafanyi biashara kuendeleza biashara bila leseni. Bw. Spika, pesa hizo zinatakikana zije moja kwa moja katika kaunti zetu ila zimezuiliwa na Serikali kuu. Hivyo basi, pesa hizo haziwezi kuja katika kaunti zetu. Bw. Spika, kuna malumbukizi ya pesa hizi. Kwa hivyo, wakikataa na kusema ya kwamba pesa hizo ziondolewe katika orodha ya fedha zinazokuja katika kaunti zetu, inakuwa ni makosa na kaunti zetu hazitaweza kutekeleza majukumu yao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}