GET /api/v0.1/hansard/entries/1483717/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1483717,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483717/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, ninaunga mkono ripoti hii na ningeomba Bunge hili liweze kuikubali na kuipitisha kwa sababu inatoa mwelekeo kuhusiana na vile ambavyo kaunti zetu zitaweza kupata fedha. Kwa sasa, karibu kwa zaidi ya miezi nne, serikali zetu za kaunti hazijaweza kupata fedha kwa sababu Mswada wa Fedha wa Mwaka 2024/2025 ulifutiliwa mbali. Sheria hii ambayo tulikuwa tumeipitisha ingesaidia pakubwa kuhakikisha ya kwamba zile fedha ndogo ndogo ambazo zilikuwa zimepangwa kupelekwa katika kaunti zimepelekwa. Asante, kwa kunipa fursa hii."
}