GET /api/v0.1/hansard/entries/1483853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1483853,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483853/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza, ninamsifu dada yetu, Fatuma Dullo, Seneta wa Isiolo, kwa kuleta malalamishi kama haya mbele ya Bunge la Seneti. Ni jambo la kusikitisha sana kuona gavana aliyeitwa kwa Bunge la Seneti aje ama gavana ameitwa na Kamati ya Seneti ajitokeze na akose kuitika. Ni jambo pia la kusikitisha kwamba, yeye kama kiongozi wa gatuzi la Isiolo, ni lazima azingatie sheria na ajue kwamba, Bunge la Seneti ndio linalomshugulikia na kumtafutia pesa ili atumie na kufanya maendeleo ndani ya Isiolo. Ule uamuzi, Bw. Spika, umeutoa hivi sasa kwamba yeye aitwe tena mbele ya Kamati, kupitia kwa Jenerali Mkuu wa polisi ni jambo nzuri. Kwa sababu, kuanzia hivi sasa, kutakuwa na heshima, itakayopeanwa kwa Maseneta wetu na Bunge la Seneti. Usipokuja Seneti, tunaweza kutumia nguvu zetu hapa Bunge la Seneti na tukamwambia Jenerali Mkuu wa Polisi ukamatwe na uletwe mbele ya Seneti au Kamati ya Seneti ili ujibu yale maswali. Tutafanya hivyo tukitumia njia hiyo na itakuvunjia heshima wewe kama gavana. Maanake, ukishikwa, utatiwa ndani korokoroni halafu siku ya pili au baada ya wikendi, utaletwa mbele ya Kamati ya Seneti ili ujibu ni kwa nini hauwezi kuja hapa. Bw. Spika, hatutaki uhusiano kama huo wa kutojitokeza wakati inapotakikana kwa serikali ya ugatuzi. Hivi sasa, tunapigania wapate pesa na hatutaki zipunguzwe na wao wanafanya tabia kama hizo. Sisi tumeona hilo si jambo nzuri. Mwisho, gavana Guyo anafaa aelewe kwamba Isiolo ni mojawapo ya serikali gatuzi na Isiolo si kipochi chake wala si nyumba yake. Anafaa aelewe kwamba Isiolo ni The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}