GET /api/v0.1/hansard/entries/1483858/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1483858,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483858/?format=api",
    "text_counter": 216,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa ninamshukuru Seneta wa Isiolo, Sen. Fatuma Dullo, kwa swali aliuliza ili tupate mwelekeo, na tumeupata. Ninamshukuru Sen. Dullo sababu amekuwa mzoefu na amekuwa kwa Seneti hii kwa muda mrefu. Swali alilouliza ni swali nzuri kwa sababu, gavana Guyo anahitajika kuja hapa katika Seneti au Kamati ya Seneti hii na kujibu maswali. Si maswali ya Seneta, ni maswali ambayo watu wa Isiolo wanataka. Wangetaka huduma na hayo ndio maswali yanayoulizwa. Bw. Spika wa Muda, imenivunja moyo sana kusikia gavana anakuja mbele ya Kamati na hakuna jambo anafanya, ila kuleta dharau katika Kamati. Nimemsikiza Seneta wa Vihiga, Sen. Osotsi, mwenyekiti wa Kamati ya CPIC akisema yule gavana, hata baada ya kufika kwa ile Kamati, alionyesha dharau. Ni kama hawafai. Maseneta, hata siku ya leo, tumekuwa tukisema kwamba pesa ambazo zinaenda kaunti zetu, ni mpaka ziongezeke. Nimemsikiza Sen. Dullo akiuliza, inawezekanaje, sisi kupigania pesa ziende gatuzi ya Isiolo, lakini gavana hawezi kuja kujibu maswali? Ninakubaliana na uamuzi uliotolewa na Spika siku ya leo, mia kwa mia. Huu mwongozo utapea wale magavana wengine wako na zile nia au tabia. Tunavyofanya katika Seneti hii ni kuwakilisha wananchi wa Kenya, katika gatuzi tulizochaguliwa. Sioni kwa nini gavana anaogopa kuja kujibu maswali, kwa sababu maswali yanayoulizwa ni kuhusu utendaji kazi wake katika kaunti yake. Kwa hivyo, asipokuja, inaonekana ni madharau na ninakubaliana na Bw. Spika, vile alivyosema kwamba, atafutwe mahali alipo, na wakati wowote Kamati itapokua ikiketi, atolewe. Hii ni kwa sababu, zile faini wamekuwa wakitozwa, kwake ni mzaha, atatoa zile pesa kwa akaunti za gatuzi zetu na alipe. Anatoa mkono huu na kuweka kwa huo mkono mwingine. Ninampongeza tena Sen. Dullo kwa kazi nzuri amefanya na ametupa mwongozo. Asante."
}