GET /api/v0.1/hansard/entries/1483876/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1483876,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483876/?format=api",
    "text_counter": 234,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Mstahiki Spika wa Muda, kwa kunipa hii nafasi. Kwanza kabisa, ni jambo la aibu kwa sababu aliye gavana wa Kaunti ya Isiolo, mhe. Abdi Guyo alikuwa Mwakilishi Wadi ya Matopeni. Wakati huo nilikuwa Mwakilishi Wadi wa Kerugoya. Mhe. Guyo, pia alikuwa Kiongozi wa Wengi kama mimi. Nilipokuja Seneti, yeye naye alifanikiwa kuwa gavana wa Kaunti ya Isiolo. Tunaamini kwamba ukifanikiwa kupanda ngazi kutoka Mbunge wa Bunge la Kaunti hadi kuwa gavana, huwa umesoma mambo mengi. Ni vibaya na aibu kuona wanaofanikiwa kupanda cheo kutoka kuwa waakilishi wadi hadi kuwa magavana, ndio wanavunja sheria. Hiyo ni kutuharibia sifa hata sisi. Pili, Seneti sio tingatinga linalotumika kutengeneza barabara mahali palipo na mawe na miti na pindi tu linapomaliza, linawekwa kando lisiharibu barabara. Tunapokuja huku kupitisha pesa zinazotumiwa na magavana, lazima wajue tutafuatilia jinsi hizo pesa zinavyotumika kufanya kazi mashinani. Kwa hivyo, gavana anapoarifiwa anafaa kufika mbele ya kamati ya Seneti, anafaa afike kwa mapema ili kujieleza. Hii sasa inaonekana kuwa kinaya na pia kukosea Seneti heshima kwa kutaa kuja hizo siku zote. Niliangalia wakati kulipokuwa na kikao cha CPISFC ambapo gavana Guyo alimtusi Seneta wa Narok. Hili sio jambo la mzaha au kufurahia. Ni tabia inayoonyesha ya kwamba, iwapo sisi hatuwezi tetea watu wa Isiolo, watatetewa na nani dhidi ya gavana anaye mtusi Seneta katika kikao cha kamati? Hivyo basi, achukuliwe hatua zifaazo. Aletwe mbele ya kamati zote anazofaa kuwajibika. Ikiwezekana, atiwe mbaroni na awe anatolewa korokoroni kuhudhuria vikao vya kamati za Seneti na kurudishwa humo hadi atakapomaliza vikao vyote. Hii ni kwa sababu hatujui kama akiachiliwa huru atahudhuria vikao vya kamati za Seneti au atatoroka. Asante sana."
}