GET /api/v0.1/hansard/entries/1483879/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1483879,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483879/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nakumbuka jana tulikubaliana kuwa kama gavana huyu hatafika mbele ya kamati, atozwe faini ya Kshs500,000. Hivyo basi, naunga mkono kuwa Mkuu wa Polisi aje mbele ya Bunge hili na atueleze kwa nini hajafanikiwa kumtia mbaroni gavana Guyo ili aweze kuja mbele ya kamati za Seneti. Mhe. Rais wa Kenya kila mwaka huja kwa Bunge na kuhutubia taifa. Kila siku ya Jumatano, Mawaziri huja kujibu maswali Bungeni. Gavana wale wengine wote huja mbele ya kamati za Seneti. Iweje sasa gavana wa Kaunti ya Isiolo peke yake hawezi kuwajibika? Napendekeza wenyeviti wote wa kamati zote husika ambazo gavana wa Kaunti ya Isiolo amedinda kuhudhuria vikao waorodheshe pamoja mashtaka dhidi ya gavana Guyo. Atakapokamatwa na Generali Mkuu wa Polisi, afikishwe hapa Seneti mbele ya Maseneta wote 67 na kusomewa mashtaka haya yote kwa pamoja. Sisi tumekuwa hapa kila mara tukiongea masuala ya ugatuzi, fedha za hospitali, shida za wafanyikazi, fedha za kuimarisha barabara zetu na miradi mingine ya maendeleo. Iwapo wakati wote tunatetea ugatuzi, basi gavana wa Kaunti ya Isiolo anapaswa kuwajibika na kuyajibu maswali yote ya katika kaunti yake. Ni jambo la kuhuzunisha sana kuona haajibiki vilivyo. Hivyo, basi, kama Seneta wa Kaunti ya Embu, naunga mkono Hoja ya kumleta gavana wa Kaunti ya Isiolo mbele ya Seneti ili achukuliwe hatua kali. Naunga mkono."
}