GET /api/v0.1/hansard/entries/1483881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1483881,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1483881/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa fursa hii. Naomba nikupongeze kwa Hoja hii muhimu sana kwa uendeshaji wa shughuli za Seneti. Mienendo ya gavana wa Isiolo sasa imekuwa donda ndugu. Mimi ni mwanachama wa Kamati ya Kudumu ya Uwiano wa Kitaifa, Usawa na Ushirikiano wa Kanda. Bunge hili katika Hoja yake ya hali halisi ya taifa baada ya maandamano ya vijana wa Gen Z tulipewa jukumu kuwaita magavana wote ili kutathmini hatua walizochukua kuhakikisha vijana wanapata nafasi za kazi na ajira katika kaunti zetu. Jambo la kusikitisha ni kwamba gavana huyu wa Isiolo mhe. Guyo amekataa katakata kufika mbele ya Kamati hii. Pia nasikia amekataa kufika mbele ya kamati zingine za Seneti. Hivyo basi, Maseneta wanafaa kutoa ilani kali kwa huyu gavana na wale wengine walio na nia ya kutoheshimu amri za Seneti. Seneti kwa mara ya kwanza imepata hadhi yake na sifa zake kedekede za kufuata sheria ya kufanikisha ugatuzi katika kaunti zetu. Niwaonye wale magavana walio na nia ya kufuata nyayo za gavana wa Isiolo, hatutazembea kazini yetu. Tutahakikisha wewe kama gavana unayepata pesa za umma ili kumhudumia mwananchi umewajibika. Ni lazima ufike kwa kamati zetu za Seneti ili ujieleze. Sio kwamba tunakushtumu. Sielewi kwa nini gavana huyo anaogopa kuja mbele ya Seneti. Ni nini anachokificha kiasi ya kwamba hawezi kuja kukieleza? Naomba hatua kali zichukuliwe dhidi yake kando na yale uliyoyasema katika ujumbe wako. Gavana huyu akamatwe ikiwezekana hata leo ili afikishwe mbele ya Bunge ajieleze tujue ni nini hasa anachokificha katika Kaunti ya Isiolo. Naunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}