GET /api/v0.1/hansard/entries/1484569/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1484569,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1484569/?format=api",
    "text_counter": 510,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Swali langu kwa mshahidi; umeelezea Bunge la Seneti kwamba, wafanyikazi wa Serikali hawakubaliwi kuchukua pesa kama zawadi. Lakini wafanyikazi wa Serikali wanakubaliwa kuchukua zawadi ya aina nyingine. Tena, ukasema katika EACC kuna orodha ya kuorodhesha kila kitu ambacho kinachukuliwa na mfanyikazi yoyote wa Serikali. Tunajua ya kwamba, Naibu wa Rais amekuwa mbele ya Kenya nzima akasema amepata ng’ombe kutoka kwa marafiki zake wa Bonde la Ufa kama zawadi. Elezea Bunge la Seneti ikiwa uko na orodha yoyote ya ng’ombe za maziwa ambazo anasema alipewa? Aliziorodhesha?"
}