GET /api/v0.1/hansard/entries/1485433/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1485433,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1485433/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu Mashariki, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Ruweida Mohamed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuchangia hii Ripoti. Haya mambo ya kuruhusu kampuni kutolipa ushuru yanafaa kufanyika kwa uangalifu sana. Kuna haja saa nyingine kampuni ipewe nafasi kuleta bidhaa bila kulipa ushuru kwa sababu bidhaa ile itamsaidia Mkenya. Kwa mfano, wakati wa Ramadhani, kule Saudia kuna matajiri Waislamu wengi wanaotoa bidhaa kama tende kuleta huku, na wanalipa nauli ya meli. Lakini bidhaa ikifika huku, mambo ya ushuru tujipange wenyewe. Hiki huwa ni chakula cha msaada. Ni tende ya kufungua saumu wakati wa Ramadhani. Inawezesha wenye huwa hawapati tende kupata. Ikiwa kuna vikwazo kuwa lazima walipe ushuru, meli inafika Mombasa na wenye uwezo wanalipa ushuru kisha wazichukue zile tende waende waziuze. Hivyo basi, wale ambao wanafaa kufikiwa na ile tende hawafikiwi. Ninaishukuru Serikali kwa kuchukua jukumu la kutoa ushuru kwani inasababisha tende ije. Hakuna atakayesema kuwa yeye ndiye alizilipia zile tende ushuru ndio aziuze, ama afanye vile anavyotaka. Inakuwa rahisi tende kufika hata mashinani ikiondolewa ushuru. Ni jambo nzuri sana, na tunataka liendelee. Ninampongeza Rais Ruto kwa kuendeleza jambo hilo tangu aingie ofisini. Vile nimepata hii nafasi na tunazungumzia jambo hili, ninaomba Serikali, kupitia Rais Ruto, ifanye mpango mapema zaidi, labda mwezi moja kabla ya Ramadhani. Saa zingine ile tende inaondolewa ushuru, lakini inachelewa kuingia, na ikifika, huwa Ramadhani imeisha. Kamati iseme kila kampuni lazima ilipe ushuru, au kila bidhaa lazima iwekewe ushuru. Hii inasaidia sana, na watu wengi wanafaidika. Hawafaidiki Waislamu peke yao; hata Wakristo wanafaidika. Kwa mfano, mimi nikigawa tende Lamu, ninawapatia Waislamu na Wakristo. Hili la Blue Nile Rolling Mills, ninataka Bunge hili tuwe waangalifu. Sikuwa kwenye Kamati, lakini nimeangalia mapendekezo yake. Ninadhani uchunguzi ulifanywa vizuri. Kama kumeonekata tatizo, basi iendelee hivyo. Lakini kama hakuna tatizo, basi isiwe ni kugandamiza tu kampuni. Tunazihitaji hizi kampuni. Zikiwa hapa zinaajiri watu ambao wanafaidika. Ninasisitiza kuondolewa kwa ushuru, kama kwa tende, kwa kuwa inatusaidia sana. Ifanywe mwezi moja au miezi miwili kabla Ramadhani. Asante, Mhe. Spika wa Muda."
}