GET /api/v0.1/hansard/entries/1487417/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1487417,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1487417/?format=api",
"text_counter": 1962,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Ningetaka kumuuliza Mhe. Mutuse swali kwa sababu kampuni nyingi ambazo ameorodhesha pale kama ushahidi ni kwamba ni za watoto wake Naibu wa Rais, Rigathi Gachagua. Kwa sababu umesema umefanya kazi kama wakili, lazima ulikuwa unafanya kazi kupitia kampuni. Je, ilikuwa ni kwa ajili ya ulaghai ukiwa na baba yako na kwamba wale watoto ambao umewaorodhesha pale, wote walitengeneza kampuni ili kulaghai pesa kupitia zile kampuni? Swali langu la pili ni kwamba, katika stakabadhi ambazo zimewekwa pale, zinaonyesha kwamba waliokuwa wanafaa kupata mgao wa shares katika kampuni, kuna wale walikuwa wanafaa kupata asilimia 30 na ile miradi ilikuwa inafaa kwenda western Kenya, haikuwa imeorodheshwa kuja Nairobi ama pahali pengine popote. Unasikia kwamba ulikuwa umegatuliwa kwa sababu umetoka Makueni na ile miradi haikuwa inakuja Makueni? Asante sana, Bw. Spika."
}