GET /api/v0.1/hansard/entries/1488248/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1488248,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488248/?format=api",
"text_counter": 345,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami nichangie huu Mswada uliotoka Bunge la Seneti wa kuongezea kaunti mgao. Ninaupinga maana kaunti zimekuwa zikitumia pesa kwa ubathirifu. Kwa ukweli, tungependa ugatuzi uinuliwe ili tuendelee mbele lakini, wanapoulizwa waeleze jinsi walivyotumia mgao wao, hawawezi kueleza vizuri. Na ndio maana kila wakati katika Bunge la Seneti, tunawaona magavana wengi wakifikishwa pale kwa minajili ya mashtaka. Hii ni kwa sababu kaunti nyingi zina utata na mchezo wa katafuna. Rasilimali na ushuru ya Wakenya lazima upewe ulinzi na tuhakikishe kuwa pesa hizo zinaingia katika miradi inayoeleweka. Sio tu magavana kupewa pesa na ilhali barabara zimetengenezwa vipande vidogo vidogo vinavyotoshana hapa mpaka pale, maji safi hamna na maji taka yametapakaa kila mahali. Siwezi nikahukumu kaunti zote maana zingine wametumia mgao wao vizuri."
}