GET /api/v0.1/hansard/entries/1488271/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1488271,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488271/?format=api",
"text_counter": 368,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa kuweza kuchangia huu Mswada wa Nyongeza ya Fedha kwa serikali za ugatuzi. Nimesimama kukubaliana na Kamati ya Bajeti kwa hali ilivyo sasa katika taifa kushindwa kupeleka fedha hizo katika serikali za ugatuzi. Ingawa kwa sasa naweza kukubaliana kwa vile hali ni ngumu kidogo, lakini wakati hali itakuwa nzuri ni vyema fedha zishuke kule mashinani kwa sababu serikali za ugatuzi zinapopata fedha, mambo mengi huendelea katika sehemu tofauti katika taifa. Hata sasa mabadiliko yale ambayo yako katika taifa ni kulingana na serikali za ugatuzi. Wakati wa zamani, fedha zote ziliwekwa katika hazina ya Serikali kuu na ilikuwa vigumu sana fedha hizo kufika mashinani. Hii ndiyo sababu unapata kwamba sehemu nyingine za nchi hii ziko nyuma na nyingine ziko mbele. Kwa hivyo, inafaa wakati mambo yako shwari, fedha zaidi zipelekwe mashinani. Ikiwezekana, Seneti ingekaa na kuhakikisha kwamba hizo fedha za nyongeza zimetengewa wawakilishi wa wadi ili ziwasaidie kufanya maendeleo kule mashinani. Wabunge wanapopeleka fedha mashinani kupitia NG-CDF, wawakilishi wa wadi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}