GET /api/v0.1/hansard/entries/1488272/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1488272,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488272/?format=api",
    "text_counter": 369,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "pia wapewe fedha wafanye miradi pamoja na serikali za ugatuzi ili watu wetu waweze kuendelea haraka na sehemu zilizobaki nyumba ziweze kuendelea kwa kasi. Hivi sasa, hali ya uchumi ni ngumu sana lakini itakapokuwa sawa, ni muhimu fedha zaidi zifike mashinani. Utulivu ulioko katika taifa umeletwa na serikali za ugatuzi. Angalau watu wanapata vibarua. Mpango wa kazi kwa vijana unatoa ajira kwa miezi miwili au mitatu, na vijana wanajisaidia. Vijana wanapokosa fedha, mambo yote yanakuwa magumu. Katika Serikali kuu, tatizo ni kwamba mambo mengi hufanywa kwa msingi wa ukabila na kuleta hali ya sintofahamu. Nimesimama hapa kusema kwamba tukubaliana kwamba hivi sasa hakuna fedha. Wale watakaochaguliwa kukaa chini baina ya Seneti na Bunge la Taifa wazungumze wakifahamu kwamba hivi sasa, hali ni ngumu. Hali itakapoanza kuwa nzuri, wapeleke fedha zaidi mashinani kusaidia ugatuzi. Hivyo basi, fedha zaidi zitawafikie wawakilishi wa wadi ndiyo nao waweze kuwa na hazina ya kujenga barabara, kuendeleza Early ChildhoodEducation (ECD), kupeleka madawati, na kusaidia kulipa karo ili watu wetu wafaidike. Magavana wasiwe na wivu na fedha za NG-CDF ama za NGAAF za akina mama. Pesa zote zinazokwenda mashinani zinawasaidia watu wetu kufukuza umaskini. Magavana wakome kupiga hazina ambazo zinasaidia kujenga barabara na kadhalika. Wabunge, magavana na wawakilishi wa wadi wafanye kazi pamoja kuwasaidia watu mashinani. Kwa sasa, nimekubaliana lakini hali ya kifedha itakapoimarika, fedha za ziada zifikishwe mashinani. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii."
}