GET /api/v0.1/hansard/entries/1488325/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1488325,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488325/?format=api",
    "text_counter": 422,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Mheshimiwa Spika wa Muda, taifa letu sasa limekumbwa na maradhi ya saratani. Kumekuwa na kesi nyingi za saratani mpaka hata watoto wadogo wako na saratani. Kwa sababu ya umaskini, watu wetu wengi wanapoteza maisha yao majumbani mwao kwa sababu hawana uwezo wa kwenda hospitali kutibiwa. Wale wanaokwenda ni wale wanaojiweza. Ukienda pale, inakuwa ni vigumu sana kupata matibabu kama huna fedha. Ijapokuwa hospitali ni za Serikali, bei ya matibabu ni ghali mpaka hata mtu haziwezi kulipa kama hana kazi au bima. Hivi sasa, idadi kubwa ya Wakenya hawana kazi na kwa hivyo, wanapopatwa na maradhi kama hayo, inakuwa hali ni nzito sana. Kesi hizo nyingi za saratani zinachangiwa na ukuzaji wa bidhaa. Katika taifa letu, tuko na Shirika la Viwango. Shirika hilo limelala na halijui kile linalokifanya. Hii ni kwa sababu mara nyingi wanatangaza kuwa tumetumia sumu wakati wananchi wameshaitumia. Wanatuelezea kuwa tumekula sukari ya sumu, na vyakula vibaya, au tumetumia mafuta ambayo hayafai, ilhali kazi yao ni kuzuia kutoka mwanzo mwananchi wa kawaida asifikiwe na bidhaa hizo zisizo salama kwa matumizi ya binadamu. Hii ni kwa sababu mwananchi wa kawaida hawana uwezo wa kujua vile bidhaa wanavyonunua viko na usalama kiasi gani."
}