GET /api/v0.1/hansard/entries/1488326/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1488326,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488326/?format=api",
    "text_counter": 423,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Nitakupa mfano, Mheshimiwa Spika wa Muda. Kuku wa gredi hupewa kemikali ili wazidi kufura. Vifurushi vya kemikali hizo vimeelezea kuwa baada ya kuku hao hupewa kemikali hizo, wasitumike kama chakula kwa siku kadhaa mpaka ile sumu itoke miilini mwao. Lakini kwa sababu Shirika la Viwango halijali Wakenya, wale kuku wanaopewa zile dawa, kesho wanapatikana kwenye soko. Mtu anamnunua kuku amechomwa, anamla kisha inamdhuru baada ya masiku kadhaa. Anapopimwa wakati wa matibabu, anaambiwa kuwa anaugua saratani. Tayari taifa letu lina gharama kubwa ya kupeleka madawa hospitalini. Wangelizuia gharama hiyo ikiwa wangeangalia sehemu ambapo nyama hiyo inatoka. Wangelichunguza ni mbolea gani inatumiwa na kwa kiasi gani. Wangelizingatia ubebaji wa nyama hiyo mpaka sokoni. Ikifika pale, je, kuna watu maalumu wanaozunguka kuangalia kama kweli bidhaa iliyokuja haitamdhuru mwananchi?"
}