GET /api/v0.1/hansard/entries/1488329/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1488329,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488329/?format=api",
    "text_counter": 426,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "ya kutosha ili watembee katika mashamba kukagua mifugo wanapokamuliwa na kuhakikisha kuwa wanakamuliwa katika mazingira mazuri. Isiwe kuwa mifugo hao wanakamuliwa na watu wamejaa matope kisha maziwa hayo yanapelekwa mahali ambapo yanauzwa. Lazima kuwe na utaratibu wa kumlinda mwananchi ili awe na uhakika. Hata watalii wakija hapa nchini na wakule vyakula bora, hiyo ni mojawapo ya njia za kuwavutia. Wanajua kuwa ukitaka kula vyakula bora, nenda Kenya. Lakini ikiwa hatutakuwa tumejipanga vizuri, basi mambo mengi yataharibika na maradhi yatakuwa mengi."
}