GET /api/v0.1/hansard/entries/1488417/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1488417,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488417/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi Kusini, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Ken Chonga",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mstahiki Spika, kwa nafasi hii uliyonipa. Mhe. Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu 44(2)(c), ninasimama kuomba Kauli kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kiidara ya Utawala na Usalama wa Taifa kuhusiana na mgogoro wa umiliki wa ardhi kati ya familia ya marehemu Bw. Kea Rimba Gona na Bw. Mahmoud Abdalla Mohamed, kuhusiana na kipande cha ardhi, LR No.MN/III783 huko Kilifi. Marehemu Bw. Kea Rimba Gona na jamaa zake wameishi kwenye kipande hicho cha ardhi kwa zaidi ya miaka 60. Hata hivyo, bila mamlaka yoyote, walifurushwa kutoka kwenye ardhi hiyo bila amri ya mahakama inayoruhusu kitendo hicho, na kinyume na makubaliano kadhaa kati ya pande hizo mbili yaliyosainiwa mwaka 2001 na 2014, ambayo yalitenga ekari tatu za ardhi hiyo kwa Bw. Gona. Ugawaji huo ulifanyika kufuatia makubaliano yaliyoidhinishwa na ofisi ya Afisa wa Wilaya katika eneo la Kikambala mwaka 2000. Hata hivyo, licha ya makubaliano hayo, Bw. Mahmoud alimfurusha Bw. Gona kutoka kwenye ardhi hiyo. Kesi ya mahakama ilifunguliwa baadaye mwaka 2019, chini ya Kesi ya ELC Nambari 99 ya mwaka 2019, ili kuamua umiliki halali wa ardhi hiyo. Baada ya kifo cha kusikitisha cha Bw. Kea Rimba Gona tarehe 19 Julai 2024, mpwa wake, Lucky Kalama Rimba, aliwasilisha ombi la kumzika baba yake kwenye ardhi hiyo yenye mgogoro. Hata hivyo, Bw. Mahmoud alizuia mazishi hayo na akaizuia familia kutekeleza taratibu za mwisho za kumzika marehemu. Kwa bahati mbaya, mwili wa marehemu bado uko The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}