GET /api/v0.1/hansard/entries/1488418/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1488418,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488418/?format=api",
    "text_counter": 49,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi Kusini, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Ken Chonga",
    "speaker": null,
    "content": "katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Pwani hadi leo. Aidha, siku ya Ijumaa, tarehe 11 Oktoba 2024, Bw. Mahmoud na mawakala wake, baadhi yao wakidaiwa kuwa maafisa wa polisi, bila sababu yoyote au kibali cha mahakama, waliifurusha familia hiyo kutoka kwenye ardhi hiyo. Kufurushwa huko kumeiwacha familia hiyo bila makaazi na kutatiza pakubwa uendeshaji wa shughuli zao za kawaida za kimaisha, iwe kikazi au kielimu. Ni kutokana na hali hii ndipo ninaomba Kauli kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kiidara ya Utawala na Usalama wa Taifa kuhusu masuala yafuatayo: 1. Sababu ya Bw. Mahmoud kuifukuza familia hiyo kutoka kwenye makaazi waliyoyakaa kwa zaidi ya miaka 60; 2. Ni lini familia hiyo itaruhusiwa kufikia kwa makaazi yao hadi umiliki wa ardhi hiyo uamuliwe na mahakama; 3. Mbona maafisa wa polisi wanaodaiwa kutoka kwa Kituo cha Polisi cha Ndonya na Mtwapa wamekuwa wakimsaidia Bw. Mahmoud kuinyanyasa familia hiyo kwa kuwanyima fursa ya kufikia ardhi hiyo, hivyo kuingilia mchakato wa haki unaoendelea mahakamani; 4. Hatua zilizowekwa ili kuhakikisha kuwa Bw. Mahmoud hachukui umiliki wa ardhi ambayo bado ina mgogoro; na 5. Ikiwa ipo mipango yoyote kutoka katika Wizara ya Utawala na Usalama wa Taifa inayokusudia kufidia familia hiyo kutokana na mateso ya kihisia na kifedha waliyopitia tangu walipofukuzwa. Ahsante, Mhe. Spika."
}