GET /api/v0.1/hansard/entries/1488501/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1488501,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488501/?format=api",
"text_counter": 132,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Mhe. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 44 (2)(c), nimesimama kuomba Kauli kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi na Miundomsingi kuhusu kukarabatiwa kwa barabara ya Mwabungo–Majimboni–Shimba Hills– Kilulu–Mrima (Nambari B98). Miundombinu bora, haswa barabara nzuri, ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi na uboreshaji wa hali ya maisha kwa kurahisisha kufikia huduma za umma kwa haraka inavyohitajika. Hata hivyo, wakazi wa Eneo Bunge la Matuga bado hawajafurahia miundomsingi kwa sababu ya hali duni ya takriban kilomita 50 za barabara ya Mwabungo– Majimboni–Shimba Hills–Kilima–Kilulu–Mrima (Nambari B98), ambayo kwa sasa iko katika hali mbaya na haipitiki. Mbali na kuunganisha sehemu nyingi inazopitia katika Kaunti ya Kwale, barabara hiyi pia hufanikisha shughuli za utalii katika Hifadhi ya Kitaifa ya Shimba Hills. Hali mbaya ya barabara hiyo imeathiri uchumi kwa kupandisha gharama ya uchukuzi, biashara na ufikiaji huduma za umma. Licha ya Mamlaka ya Barabara Kuu ya Kenya (KeNHA) The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}