GET /api/v0.1/hansard/entries/1488502/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1488502,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488502/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Mhe. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "kutangaza Zabuni Nambari KeNHA/R9/150/2024 ya kukarabati barabara hiyo mwezi wa Februari 2024, hakuna hatua yoyote dhahiri ambayo imechukuliwa hadi sasa – hali ambayo inazua wasiwasi miongoni mwa wakaazi kuhusu utekelezaji wa zabuni hiyo. Mhe. Spika, kutokana na hali hiyo, naomba Kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi na Miundomsingi kuhusu yafuatayo: 1. Ripoti kuhusu hatua zilizoafikiwa katika utekelezaji wa Zabuni Nambari KeNHA/R9/150/2024 iliyotangazwa mwezi wa Februari 2024 kuhusu ukarabati wa barabara ya Mwabungo–Majimboni–Shimba Hills–Kilulu– Mrima (Nambari B98). 2. Hatua zinazochukuliwa ili kukarabati barabara ya Mwabungo–Majimboni– Shimba Hills–Kilulu–Mrima (Nambari B98) haraka iwezekananvyo, ikiwa ni pamoja na kiwango cha fedha zilizotengewa mradi huo. 3. Mipango iliyowekwa na KeNHA ili kuweka lami barabara ya Mwabungo– Majimboni–Shimba Hills–Kilulu–Mrima, ikiwa ni pamoja na ratiba ya ujenzi wa barabara hiyo na tarehe ya kukamilishwa. Asante, Mhe. Spika."
}