GET /api/v0.1/hansard/entries/1488504/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1488504,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488504/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Msambweni, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Feisal Bader",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi. Ningependa kuongeza sauti yangu kwenye suala ambalo Mhe. Tandaza ameeleza. Hii ni barabara muhimu sana inayounganisha maeneo bunge matatu katika Kaunti ya Kwale. Hii barabara inaanzia katika Eneo Bunge la Msambweni, ambalo ninawakilisha hapa. Inapitia Eneo Bunge la Matuga, linalowakilishwa na Mhe. Tandaza, hadi Eneo Bunge la Lungalunga. Barabara hii ni kama imesahauliwa na shirika la KeNHA. Kama tunavyojua, miundombinu ndio uti wa mgongo wa maendeleo. Katika Kaunti ya Kwale, hizi ndizo sehemu ambazo tumezingatia pakubwa suala nzima la ukulima. Kwa mfano, katika sehemu ya Shimba Hills, kuna watu wanaofanya ukulima. Ni sehemu ambayo machungwa yanakuzwa kwa wingi sana. Asilimia 70 ya machungwa tunayotumia katika Mkoa wa Pwani yanatoka katika eneo la Shimba Hills, ilhali barabara yake haipitiki. Kwa hivyo, hata mimi ninamuomba Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi na Miundomsingi aje hapa atueleze Wizara imeweka mikakati gani ya kuhakikisha kwamba barabara hii inakarabatiwa kwa haraka upesi. Asante sana, Mhe. Spika."
}