GET /api/v0.1/hansard/entries/1488930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1488930,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488930/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika, naunga mkono Hoja hii ili tuwe na nafasi ya kumsikiliza Naibu wa Rais siku ya Jumamosi. Tunaelewa kwamba hii ni kesi muhimu sana na macho yote nchini yanaangalia Seneti. Napeana pole zangu kupitia Senior Counsel, Mhe. Paul Muite, kwa sababu client wake ni mgonjwa. Ugonjwa ni jambo la Mwenyezi Mungu. Hatuwezi kusema kwamba mtu hawezi kuwa mgonjwa. Mtu yeyote anaweza kuwa mgonjwa. Kwa hivyo, ningependa afikishe pole za Seneti. Tunamtakia kila la heri. Mwenyezi Mungu ampe nafuu ili tupatane hapa. Bw. Spika, tuko katika njia panda; ni mgonjwa. Je, tuendelee ama tusiendelee? Tumpe nafasi. Kama binadamu, hii ni nafasi nzuri ya kuonyesha ubinadamu kama Maseneta ama Seneti. Tumpe nafasi akiwa hospitalini ili aweze kupata nafuu anapoendelea kupokea matibabu. Hoja hii imekuja wakati mwafaka. Kwa hivyo, tumpe nafasi. Naunga mkono Hoja hii."
}