GET /api/v0.1/hansard/entries/1488954/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1488954,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488954/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Zamzam Mohamed",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, kama mwakilishi wa eneo Kaunti ya Mombasa na Bunge la Taifa ya Kenya. Leo nimekuja hapa kuwaletea yale mashtaka ambayo yameonekana katika Bunge yetu. Mengi yamezungumzwa. Mimi sio mwanasheria lakini nazungumza kama Mkenya ambaye yuko pale chini, hajui sheria lakini anaomba amani. Video zimechezwa katika Bunge hili, tumeona Naibu Rais akijipiga kifua, hasa kule Taita-Taveta nimeona akiwaambia kuwa hawana shares. Na akawaambia kama wanataka hisa wangoje 2027, kwani hata Rais akieleza Naibu wake alete maendeleo nitamwambia asubiri aangalie mfuko wake kwenye orodha ya kupewa maendeleo. Ifahamike kuna wakati moja Kenya iliingia kwenye vita. Tuliona maiti ya kina mama, mtoto hajui mama amekufa, alikuwa ananyonya matiti. Hatuwezi kutaka taifa hili lirudi kule tena. Ndani ya Mombasa nina wajane ambao wananitegemea. Waliniletea malilio yao. Leo mimi kama mama Kaunti wa Mombasa nalia kwa sababu ya mayatima ambao waliwachwa na ndugu wa Naibu Rais. Haiwezekani kuwa leo mimi na mume wangu tutafute mali yetu na tuna watoto wetu, kisha akifa aende mbele ya Mwenyezi Mungu nije nipokonywe mali yangu niachwe na watoto wangu wakihangaika. Ukiangalia umri wa watoto wa ndugu yake Naibu Rais wametoshea kupewa uridhi wao. Lakini hata kuna tetesi kuwa mwingine anaozea kule kwa jela. Nilisikia mwanasheria akisema tu-save makanga, mimi nasema makanga ameiba pesa ya abiria, dereva hana pesa ya kupelekea mwenye gari. Wamwache dereva apeleke abiria mpaka stesheni ya mwisho. Ikifika kule atajua atatafuta makanga mwingine namna gani. Hatuna uchungu na watu wa ‘mlima’ lakini tunachosema tulikuwa na Uhuru, Kibaki na Kenyatta, lakini hatukuwahi ona mambo ambayo tumeona kwa DeputyPresident. Huyu ni sumu, atavuruga Kenya, ataharibu Kenya. Naomba Bunge hili la Seneti, amani ya Kenya iko kwenye mikono yenu. Naomba mtoe uamuzi wa uhakika. Huyu jamaa hapendezi kisa kuwa katika nafasi ambayo yuko ndani sasa. Nawaomba kwa heshima na taadhima tuweze kumpandua mamlakani leo ili Kenya iwezekupata mtu ambaye atamsaidia Rais kufanya kazi akiwa ameweka amani na umoja wa Wakenya mbele. Asante Bw. Spika."
}