GET /api/v0.1/hansard/entries/1488999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1488999,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1488999/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Spika. Naunga mkono Hoja hii inayohusu kumng’atua mamlakani Naibu wa Rais. Katika Kanuni zetu za Kudumu, Kipengele 145, kinaongea jinsi Rais ama Naibu Rais anavyoweza kuondolewa mamlakani. Kwanza, mashtaka yote yalioko mbele yetu kuhusu ukosefu wa nidhamu au nidhamu kwa Wakenya, inasikitisha kusikia Naibu Rais akisema kwamba Kenya ni kampuni na kwamba iko na hisa na kama hukuwapigia kura kama walivyotaka, utangojea sana kupata maendeleo. Mtu akiwa Naibu Rais anakuwa kiungo muhimu cha kuunganisha taifa. Ukiwa Naibu Rais uliyechaguliwa, maendeleo ni lazima yafike mashinani kote nchini kwa waliokupigia kura na hata wale ambao hawakukupigia kura. Wewe ni kama ndugu, baba, babu na mzee wa nchi hii. Kila unapoenda katika nchi yetu unafaa kuheshimika. Jambo la kusikitisha ni kwamba hajaongea hivyo mara moja au mbili, pengine tungesema ulimi uliteleza. Katika hii miaka miwili yeye akiwa Naibu Rais, kila siku mahali popote alipoenda amehubiri maneno haya. Hata ameenda maeneo ya ndugu yangu, Sen. Cherarkey, ambaye ni Mkenya halisi na akatamka tena maneno hayo; maneno ya kutenganisha Wakenya kwamba sisi ndio tumepata kwa hiyo wale wengine watabaki. Nchi ya Kenya ni moja na kila mtu analipa ushuru. Pia, sisi tunaotoka pande za Pwani, Kisumu, Western na kila mahali Kenya hii tunalipa ushuru. Kwa maoni yangu, ni jambo la kusikitisha kuona kwamba Naibu Rais akitamka kwamba Kenya ni kampuni na lazima uwe na hisa za kutosha kupata maendeleo. Vilevile, nitaongea kuhusu ninakotoka Kilifi, mahali panaitwa Vipingo. Hapo ni mahali ambapo yeye ana hoteli ya familia. Hoteli ilikuwa ya ndugu yake lakini hatimaye akaichukua. Kitu cha kusikitisha ni kwamba watu wa Kilifi tunahitaji maendeleo ya barabara sana. Mojawapo wa mambo tunayolalamikia zaidi upande ule ni kwamba barabara ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}