GET /api/v0.1/hansard/entries/1489000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1489000,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1489000/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "kutoka Mombasa hadi Malindi iligeuzwa katikati na ikaenda kwa hoteli inayoitwa Vipingo Beach Resort Limited. Huo ni mradi ambao ungefaidisha zaidi watu wa Kilifi hususan wakulima, wafanyibiashara na wananchi lakini yeye akaigeuza ikaenda kwake. Nilipata fursa ya kuenda huko. Barabara hiyo imehepa mikanju na miembe ikienda kwenye hiyo hoteli. Hivyo sio namna barabara zinavyotengenezwa. Huo ni ukiukaji wa nidhamu. Mhe. Spika, sisi sote tunaamini kwamba kuna Mungu na ukimkosea atakuadhibu wakati fulani. Wale waliokosewa sasa hivi, kuna malipo yanayoendelea. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba ukifa mali yako haitaenda kwa watoto wako bali kwa ndugu yako na bibi yake na watoto wake. Huo ni ukosefu wa nidhamu. Kama kiongozi wa familia, unatakiwa uilinde na kuitunza na kuhakikisha wamepata maendeleo. Wajane wanapolia, Mwenyezi Mungu hujibu na wakati wake wa kujibu umefika. Asilaumu mtu yeyote. Bunge hili halina upendeleo wa upande wowote. Tunasema haki itendeke. Mwisho, kama unaketi katika Baraza la Mawaziri, yeye akiwa mmoja ya wale watu wanaosimamia National Intelligence Service (NIS), alitamka mambo yasiyofaa ya kulaumu Kiongozi wa Ujasusi. Kama alikuwa na nia ya kusema kitendo hicho, angemuita Kamshina wa Polisi na Mkuu wa Ujasusi na kuwaketisha pamoja. Angehoji Mkuu wa Ujasusi kama alipeleka ripoti yake kwa Kamshina wa Polisi. Lakini kuenda kwa mkutano wa hadhara na kusema mtu fulani hafanyi kazi ipasavyo kwa ofisi yake ni kosa sana. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana na huwezi kuficha siri ya yale yanayotendeka katika kazi zao za ujasusi. Kwa vile nimeona ile njia ambayo ameelekea na kazi zake, hauelekei kisawasawa. Kwa maoni yangu na najua pia ndio maoni ya wengi, nimeonelea kwamba, zile sababu zililetwa hapa, alikosea utendakazi wake na aondolewe katika mamlaka. Ninaunga hoja hii. Asante, Bw. Spika."
}