GET /api/v0.1/hansard/entries/1489054/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1489054,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1489054/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Kwanza ningetaka kumuombea afueni haraka Naibu wa Rais. Ningependa kusema hivi, fisi anapotaka kula mwanawe, husema kwamba ananuka kama mbuzi. Ni dhahiri shairi kuwa, mashtaka iliyo mbele yetu leo ni fisi anayetaka kumla mwanawe. Wakati Sen. Thang’wa alikuwa anaongeo hapa, leo ulimwambia uombe msamaha. Alikuwa amemwambia Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Jinai kwamba anapojibu, ajibu na wanao. Mashtaka ambayo imekuwa na kampuni zote zilizokuwa hapa, mingi zilikuwa za watoto wake Rigathi Gachagua. Ama kweli, chambilecho, mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu. Kwa sababu hakuwezi kuwa na ubaguzi wa wanawe Naibu Rais, lakini kusiwe wale wengine wanaopewa heshima tofauti na hiyo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}