GET /api/v0.1/hansard/entries/1489055/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1489055,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1489055/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Mimi nimetoka Kirinyaga na ninajua mashtaka yote 11 ambayo yako hapa. Kuna jambo moja ambalo mpaka ufanye kama utadhihirisha hayo mashtaka na ni ushiriki wa umma ambao tuko na ushahidi mbele yetu. Katika ushirika wa umma ambao tuko nao mbele yetu, isipokuwa picha za maofisi za National Government – Constituency Development Fund (NG –CDF) na takwimu ambazo zimetoka katika Bunge la Kitaifa. Hii ni kwamba wale wote ambao walikuwa wametia sahihi kumuondoa Naibu wa Rais ndio walio ongoza katika ushiriki wa umma. Bw. Spika, ningeuliza itakuwaaje na itawezekanaje mtu ambaye ametia sahihi kumuondoa Naibu wa Rais anaongoza katika ushiriki wa umma? Mbuzi atapata haki wapi katika mahakama ya fisi? Ningependa kusema ya kwamba ni rahisi kuangalia mashtaka na kuyaona kama inavyofaa kwa Naibu wa Rais ambaye ako hospitali. Najua ya kwamba naweza kuwa nimesimama hapa na ninapoteza kuni nikichemsha mawe. Najua hivyo. Lakini fisi aliambia mawe siku moja, ‘hata kama haujaongea umesikia kile nimesema.’’ Katika mashtaka yaliyo hapa na sisi tunafaa kuongozwa na ushahidi sio riwaya, hekaya za abunwasi au fasihi’ Lakini tunazo hapa zote ni hekaya za abunwasi. Hakuna ushahidi wowote ambao tumepewa mbele yetu. Kwa hivyo, siwezi kusimama hapa halafu niweze kumhukumu Naibu wa Rais. Katika Kitabu ya Wakolosai 3:12 inasema ukihukumu wengine, wahukumu vile wewe utataka kuhukumiwa. Bw. Spika, sasa hii leo, tunafaa kuwaaminiaje waliyorodhesha mashtaka yaliyo hapa na kukosa kuleta ushahidi? Ni chuki ama ni uchungu gani ambao wako nayo na Naibu wa Rais. Ujuavyo, akuchukiaye huwa anakuambia unamtifulia vumbi hata wakati unaogelea. Mahali nilikotoka, kitu ya kwanza nataka kufanya ni kuwakilisha watu wangu. Waliniambia ya kwamba hawakuhusishwa vilivyo katika ushiriki wa umma ambao uko hapa. Hii ni kwa sababu waliyoenda kule mashinani kufanya ushiriki wa umma, walienda kufanya ushiriki wa umma wakijua matokeo yake. Kwa hivyo, mimi nimeambiwa na watu wangu kutoka Kirinyaga kwamba tumekuchagua wewe uende pale utuwakilishe, tafadhali ukienda, usikubaliane na yale mashtaka yote ambayo yamewekwa hapo. Bw. Spika, Mswahili husema; “lililompata peku na ungo ni lilo.” Wewe ni Mswali na unajua kwamba ‘ungo’ ni uteo ambao ni mpya. ‘Peku’ ni uteo unaopepetea ambao ni nzee. Nawaambia siku ya leo Maseneta, tukimhukumu Naibu ya Rais, yanayompata leo, hata nyinyi mjue siku moja yanawezakumpata, na ambaye atachukua msumari wa kwanza kumpigilia Naibu wa Rais, ningeomba kwamba asiwe ni mtu kutoka kwa mlima. Huyu ni ndugu yetu na tunapokuja kumsulubisha msalabani, afadhali tuangalie akisulubiwa lakini mmoja wetu asichukuwe msumari na nyundo kuenda kumsulubu. Bw. Spika, najua ya kwamba kuna wale ambao wanaelekeza vingine visivyo. Mswahili husema, “usiwe vita tange kuwatosa wengine ndemani.” Kama uko na msimamo tayari, usije ukapeleka mwenzako katika huo msimamo wako. Tunafaa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}