GET /api/v0.1/hansard/entries/1489070/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1489070,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1489070/?format=api",
    "text_counter": 288,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kumbandua Naibu Rais kwa nafasi yake ya kuwa Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya. Kwanza, na jiunga na wenzangu kumtakia afueni ya haraka Naibu Rais. Ilikuwa ni matarajio yetu kwamba jioni ya leo atakuwa hapa kujitetea kwa madai kadhaa aliyoletewa katika Bunge hili ili kutakasa jina lake. Bw. Spika, nimeangalia mashtaka yote 11. Baadhi ya mashtaka yaliyonigusa ni shtaka la kwanza. Anasema kwamba Kenya ina hisa na kwake wenye hisa ni wale waliopigia kura Kenya Kwanza katika uchaguzi wa mwaka 2022. Hiyo imebagua makabila zaidi ya 47 katika nchi yetu. Sisi tunaotoka Pwani ambapo kutoka mwanzo Pwani ilikuwa sio koloni ya Kenya, ilitupa mshtuko mkubwa kwa sababu tumeona kwamba tunazidi kutengwa katika Jamhuri yetu ya Kenya. Shtaka la pili lililonigusa ni kuhusu ukiukaji wa sheria. Nitaangazia shtaka la pili na sita ambapo amekiuka sheria unayohusu uwiano katika nchi yetu ya Kenya na kuleta makabila na jamii zote pamoja. Shtaka la tatu ni ukosefu wa nidhamu kwa kumshambulia hadharani mkurugenzi wa shirika la ujasusu nchini. Hii ilitokea mnamo 26/06/2024 ambapo Naibu Rais alikuwa Mombasa na akatoa taarifa kwamba zilizohujumu usalama wa taifa. Kama Naibu Rais alikuwa na fursa ya kuzungumzia mambo haya Serikalini na hatua za kurekebisha zikachukuliwa. Mhe. Spika, ninapoangalia makosa yote, haya yasingeweza kumfika Naibu Rais kwa sasa kwani masuala yote yaliyoangaziwa hapa, yaliangaziwa na Sen. Sifuna alipoleta Hoja yake wa kumkosoa Naibu Rais lakini Hoja ile ilikufa ndani ya Seneti. Masuala ya ukiukaji wa kiapo hayana nguvu kwa sababu alipoapishwa siku ya kwanza aliapa viapo viwili. Hatujui ni kiapo kipi alikiuka wakati Mhe. Mutuse alileta mashtaka haya. Nikimalizia nitamnukuu Sen. Orengo aliposema kaika Bunge lililopita kwamba mapinduzi yanakula watoto wao. Kwa kiingereza, Revolutions eat their own children . Tunaona mapinduzi yameanza kula watoto wa Kenya Kwanza yakianza na mtoto mkubwa ambaye ni Naibu Rais. Haya ni masuala yameendelea katika Bunge hili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}