GET /api/v0.1/hansard/entries/1489619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1489619,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1489619/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Nachukuwa nafasi hii kwa niaba yangu, eneo Bunge la Likoni na watu wa Mombasa kutoa risala za rambirambi kwa mwenda zake, dada yetu, Beatrice Nkatha. Tulikuwa naye katika hili Bunge la Kitaifa. Mhe. Naibu Spika, Mhe. Nkatha alikuwa kiongozi ambaye alikuwa na furaha na bashasha kila wakati ukimwona. Alikuwa na msimamo dhabiti wa kutetea chama chake na Kiongozi wake. Tulikuwa tunajua dada yetu ataingia katika uongozi ambao tunauita kwa Kiingereza Chief Administrative Secretary (CAS). Lakini kwa yale mambo yaliyotokea, hakuweza kufika hapo. Tunasikitika sana. Hata nimetamautishwa kusikia alikuwa mgonjwa kwa muda mfupi, takriban kama miezi miwili hivi. Tungekuwa tunajua, haswa sisi kama akina mama, tungemtembelea na kumuombea dua ili Mungu ampatie afueni. Lakini tunajua kwamba tulimpenda, lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi. Wakati mmoja nilikuwa na Mhe. Beatrice katika kamati moja. Nilikuwa karibu sana na yeye. Nilipenda sana mavazi yake. Alipovaa, alikuwa mama maridadi sana. Kile kibeti alichokibeba, viatu na nguo alizovaa zilikuwa zinawiana. Yaani alikuwa mama mtanashati sana. Hakuwa na fujo wala dhiki na mtu. Pia, tulikuwa akina mama wa kwanza katika kiti cha kuwakilisha katika kaunti zetu. Nilikuwa kule Mombasa na yeye alikuwa akiwakilisha kule sehemu ya kwao. Tulikuwa wa kwanza baada ya kupata Katiba mpya ya taifa letu la Kenya. Tunasikitika na tunaomboleza pamoja na ndugu zetu wa sehemu za Meru na Tharaka- Nithi kwa kumpoteza shujaa na dada yetu, Mhe. Beatrice Nkatha. Tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Tunaomba Serikali ya Kenya Kwanza, kupitia Daktari William Samoei Ruto, iangalie familia yake. Alikuwa kiongozi wake shujaa na mwenye msimamo. Yeye ni mwenda zake sasa, lakini najua ana watoto na pengine wajukuu. Tusiwatupe viongozi wetu wakati wamepatwa na misiba. Pia tuwakumbuke wale aliowaacha. Tunamuombea Mola amueke pema na penye waja wema. Poleni sana watu wa Tharaka-Nithi na Meru, na Bunge la Taifa na Kenya kwa jumla. Ahsante sana, Mhe. Naibu wa Spika."
}