GET /api/v0.1/hansard/entries/1489949/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1489949,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1489949/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "(CHPs) kwa Kiingereza hawajalipwa. Wanasononeka wakizunguka ilhali wanafanya kazi nzuri. Seneti ilikuwa imewatengea Shilingi 5.2 bilioni ila wale wa Bunge la Kitaifa wakapunguza bila kutazama kazi nzuri ya afya wanayofanya pale nyanjani. Kumbuka hii ni sehemu kubwa iliyotengwa na hawa ndio tutakaowategemea kwa sababu kabla ya mtu kwenda hospitali, anapaswa kuonekana na hawa maofisaa wa afya wa nyanjani. Ila pesa iliyotengwa ya shilingi 5.2 bilioni imepunguzwa hadi shilingi 2.5 bilioni. Ningetaka tusimame kidete. Walio katika Kamati ya Mshikamano wa Kitaifa, fursa sawa na utangamano wa kikanda wasibanduke. Wakae vile Seneti imesema kwa sababu kazi kuu ya seneti ni kulinda na kutetea gatuzi letu. Mtu yeyote katika Jamhuri ya Kenya atakueleza kwamba ukitembea katika gatuzi zetu, utashuhudia kazi ambayo imefanywa. Pengine mahali ambapo hakungetengenezwa barabara kunapatikana barabara. Daraja inaonekana kutengenezwa na gatuzi zetu. Hali ya afya katika sehemu zingine imeimarishwa na gatuzi zetu. Ikiwa hatutawapa fedha zozote, tutakuwa tumezembea kama Seneti na kulemewa katika kazi yetu. Ninajua kwamba Kamati inayoongozwa na Seneta Roba pamoja na wanakamati wengine wamefanya kazi nzuri. Wanaotaka kutukata miguu ni hili Bunge la Kitaifa. Naunga mkono na asante kwa Kamati yetu ya Seneti ya Fedha na Bajeti ambayo ilifanya kazi nzuri."
}