GET /api/v0.1/hansard/entries/1489967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1489967,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1489967/?format=api",
"text_counter": 112,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Ripoti ya Seneti kuhusu makadirio ya fedha ambayo tumeisoma hivi sasa katika Seneti. Muda mchache uliopita, niliuliza maswali hususan kandarasi za madaktari mashinani, malipo ya madaktari mashinani na mazingira ambayo madaktari wanafanya kazi katika Kaunti ya Bungoma. Nilipouliza maswali haya, misururu ya maswali yalichipuka kutoka kaunti mbalimbali humu Kenya, ikiwemo kwamba madaktari mashinani Kenya nzima, kwa zaidi ya miezi kumi hawajapata marupurupu yao. Leo nimeona kiini cha shida za madaktari mashinani. Kuna viongozi katika jumba fulani hapa Kenya ambao wanadhani wana uwezo wa kuhujumu, kuwatesa na kuwagandamiza madaktari mashinani kwamba hawalipi ushuru na hakuna kazi wanafanya. Naomba Seneti isimame kidete kuhakikisha kwamba fedha ambazo Wakenya wanatozwa kama ushuru zinatumika kuwalipa madaktari mashinani ili kuboresha afya katika zahanati na hospitali za Kenya. Vilevile madaktari waliobobea na wenye tajriba na wako tayari kufanya kazi kuandikwa kazi. Bi. Spika wa Muda, kupunguzwa kwa fedha zinazoenda katika kaunti ni kusema kwamba shule za chekechea na vyuo anuai katika nchi ya Kenya havitaweza kuimarishwa au kujengwa na watoto wetu kupata masomo jinsi ilivyopangwa katika uasisi wa ugatuzi. Naomba Wakenya waangalie Seneti. Hatutatishwa wala kuyumbayumba. Tutahakikisha kwamba ugatuzi unawajibikiwa. Na jinsi tunavyotetea magavana kupata pesa, lazima waje hapa kutueleza walivyowajibika kutumia hela hizo. Isiwe kama tunatoa ilani wa inspecta generali kama The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}