GET /api/v0.1/hansard/entries/1489968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1489968,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1489968/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "tulivyotoa juzi kwamba Gavana wa Isiolo akamatwe na kuletwa mzimamzima ili kujibu maswala ya uwajibikaji. Bi. Spika wa Muda, miundo mbinu kama barabara katika nchi ya Kenya zinahitaji fedha. Hatuwezi kusema magavana na viongozi wa kata, Members of County Assemblies(MCAs) wachukue jembe na vifaa mbalimbali waende kutengeneza barabara. Lazima Serikali ihakikishe mabilioni ya pesa wanayopunguza kutoka mapendekezo tuliyopeana ya zaidi ya Shilingi 400 bilioni zitolewe ili tujenge barabara na vivukio ili Wakenya waweze kufurahia matokeo ya jasho lao. Nikimalizia, Wakenya waliandamana na kuleta bugdha katika baraste na nchi nzima wakitaka uwajibikaji, utendakazi na uwazi. Kama Seneti kazi yetu ni kulinda ugatuzi, kutetea kaunti zetu na kuhakikisha kwamba mgao unaoenda katika kaunti uwe unaweza kutumika kuimarisha maisha ya wakenya. Katika sekta ya ukulima, Serikali imekuwa inatoa pembejeo lakini mfumo mzima wa ukulima ama zaraa katika nchi ya Kenya unayumbayumba. Hii ni kwa sababu wanategemea wahisani lakini hawana nguvu za kinishati za kuenda mashinani na kujihushisha na kuwapa moyo na ujuzi wakulima na kuboresha mavuno ya wakulima, ikiwemo wakulima wa kahawa, majani chai na miwa. Kuna Mswada unaohusu miwa tumeuleta leo Bungeni. Serikali za kaunti hazijapata nguvu kwa sababu Serikali ya Kitaifa imekataa kuachilia pesa ili magavana na watendakazi katika kaunti waweze kuimarisha kilimo katika nchi ya Kenya. Bi. Spika wa mda, tunapogatua michezo na sanaa na kaunti hazijaweka katika migao yao ya uchapakazi pesa za kuimarisha michezo na sanaa, itakuwaje tutarajie matokeo pale mashinani. Naomba pesa tulizodai ziende kwa kaunti kama Seneti zitolewe. Tutawaandama magavana wachapakazi waweze kuimarisha michezo na usanii ili vijana wapate kazi na wale ambao si wazembe wapate kipato na Kenya isonge mbele kwa jumla. Kwa hayo, naunga mkono msimamo wa Kamati ya Seneti kwamba Serikali ama Bunge la Kitaifa lituachie nafasi na litende haki kwa wakenya jinsi tulivyotoa mapendekezo yetu kama Seneti kwamba pesa zisipungue bali zibaki zaidi ya bilioni mia nne. Asante."
}