GET /api/v0.1/hansard/entries/1490297/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1490297,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1490297/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa na Seneta Hamida. Maswala ya afya yanazidi kudorora katika kaunti zetu. Sio Mama Lucy Kibaki Hospital peke ambapo huduma zimelemaa na kuwa na ukosefu wa fedha. Tunapozungumza sasa hivi, hospitali ya Mrima, Likoni, Kaunti ya Mombasa, kina mama waliojifungua wamezuiliwa katika hospitali hiyo kwa sababu hawajalipa gharama za kujifungua. Mradi wa Linda Mama ulikua unasaidia kina mama kujifungua katika hospitali zetu na mbali na kutolipishwa, walikua wakitoka hospitali na zawadi ndogo ndogo za kusaidia maisha yao. Kwa hivyo, kuna umuhimu wa hili swala la afya kuangaliwa kwa undani zaidi. Kila tunapochelewa kumaliza maswala ya Division of Revenue Act (DORA), ina maana kwamba, fedha zitaendelea kuchelewa katika kaunti zetu na huduma zitaendelea kudorora. Bw. Spika, kuna malipo ya National Health Insurance Fund (NHIF) ambayo sasa inaitwa Social Health Insurance Fund (SHIF) yamesimamishwa kwa sababu hospitali hazilipi malimbikizo ya pesa zinazodaiwa. Ni muhimu Waziri wa Afya kuja hapa Bunge hili kueleza ni kwa sababu gani mradi wa Linda Mama umesimama na ni lini watalipa malimbikizo ya pesa ya NHIF ili hospitali zetu ziendelee kutoa huduma kwa wananchi bila matatizo."
}