GET /api/v0.1/hansard/entries/1490487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1490487,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1490487/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii nitoe maoni yangu kuhusu sheria hii mpya. Natangaza kutoka Seneti leo kwamba hii sheria inatangaza mwanzo mpya kwa sekta ya maji Kenya. Tumetengeneza sheria ya kuwezesha wawekezaji wa kibinafsi ambao watashirikiana na serikali gatuzi na mashirika mengine ya serikali yanayohusika na mambo ya maji ili kuboresha utoaji wa maji kwa wananchi wa Kenya katika gatuzi zote 47. Bi. Spika wa Muda, wananchi wa Kenya wanakumbuka katika historia ya Kenya kwamba miaka iliyopita Serikali ilikuwa inafanya kila kitu. Mtu akiajiriwa alikuwa anapewa nyumba na gari, na wale ambao mamlaka yao hayaruhusu kupewa gari walipewa usafiri wa basi ili kumchukua mtu na kumpeleka kazini na kumrudisha nyumbani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}