GET /api/v0.1/hansard/entries/1490488/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1490488,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1490488/?format=api",
"text_counter": 301,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kampuni za kibinafsi zilizokuwa wakati tuko watoto kama Kenya Ports Authority (KPA) na Kenya Breweries Limited (KBL) zilikuwa zinajengea wafanyakazi wao nyumba na kuhakikisha kwamba wana usafiri wa basi wa kuwapeleka kazini na kuwarudisha nyumbani. Jinsi miaka imeenda, mambo yalianza kugeuka ikawa kwamba haiwezekani Serikali kupatia kila mtu gari. Wawekezaji wa kibinafsi wakaanza kuingia kwa sekta hiyo. Mtu akiajiriwa, ikawa kwamba sio serikali inayotafutia watu usafiri wa kuenda kazini, bali wawekezaji wa kibinasi. Watu wakaanza kulipa nauli kuenda kazini na kama kwako ni karibu na kazi, unatembea kwa mguu. Mambo yakazidi kubadilika kwa watu waliokuwa wanategemea Serikali kuwapatia nyumba. Wawekezaji waliingia wakawa wanakodisha nyumba kwa wafanyakazi wa Serikali kwa sababu nyumba za Serikali zilikuwa hazitoshi. Uwezo wa Serikali ulizidi kuwa mfupi. Makampuni makubwa kama KPA yakaanza kutoa nafasi za nyumba lakini unakosa kupewa allowance . Ukipewa allowance, ulifaa kukodisha kwa wawekezaji. Kwa hivyo, mambo yamebadilika. Bi. Spika wa Muda, leo hii tunazungumzia sekta ya maji. Wananchi siku zote wanauliza kwa nini hakuna maji miferejini. Ukweli ni kwamba hata tukipinga hizi kampuni mpaka mwisho, kuna shida ya kiasili. Ndio, kuna shida ya management, lakini shida ya asili ni kwamba ile mifereji ya zamani haitoshelezi haja za wananchi wa sasa. Hii ni kwa sababu watu wameongezeka na mifereji iliyotengenezwa na manispaa ya zamani ishazeeka na mingine imepasuka na hali ya maisha imegeuka. Sasa hivi tumeingilia sekta ya maji na tuko na mwanzo mpya. Tukishapitisha hii sheria, uwekezaji wa kibinafsi utaingia kwa kaunti zetu zote na mashirika ya serikali. Watu watashirikiana na serikali gatuzi ili kuweka fedha zao na kusimamia mipango ambayo italeta maji ambayo tumetafuta kwa miaka mingi. Kwa hivyo, wale wanabiashara wanaosikiliza kikao cha Seneti leo watafute njia. Sisi wabunge wa Seneti na Bunge la kitaifa tutapitisha sheria hii. Tuna imani ya kwamba tukishaikagua na kumalizana nayo ikienda kwa Raisi, itapita kwani ni lazima atie sahihi. Mwanabiashara ambaye amekuwa na shida ya maji, na kuteka maji na mikokoteni, hivi sasa tunawashauri watoke kwenye biashara hizi. Tunabadilisha sheria ili wawekezaji wa biashara za maji wafaidike. Wanabiashara hawa washikane na Kaunti ili waweze kupata pesa kidogo kutoka kwa wananchi wanaoletea maji na mikokoteni, gari ama geleni. Wanabiashara hawa waingie kwenye serikali za kaunti na kupata hela kidogo kutoka kwa hii kazi. Ikiwa wawekezaji hapa nchini wataingia kwenye sekta hii, sawasawa na vile watu wa matatu waliingilia sekta ya uchukuzi, wawekezaji wakiingia kwenye sekta hii kama wale wa nyumba za wananchi na wafanyikazi ambao walikuwa wanategemea serikali--- Watu waliowekeza kwa nyumba hawasemi wamekosa kitu. Watu ambao watafungua macho yao na kwenda kwa serikali za kaunti na kuangalia sehemu ya Nairobi na Tana River wanaweza fanya kazi, hii inaweza kuwa biashara utakayo fanya pamoja na watoto wako. Wakiondoka duniani, wajukuu wako watafanya pia na vilevile vitukuu. Maji ni uhai na hakuna siku ambayo watu watasema hawataki maji. Ukweli wa mambo ni kwamba, katika nchi ambazo zimeendelea kama Ujeremani, nilipata nafasi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}