GET /api/v0.1/hansard/entries/1490489/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1490489,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1490489/?format=api",
"text_counter": 302,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "nikaenda mji wa Munich. Baada ya mikutano tulikutana mzee mmoja ambaye anasimamia kampuni ya kusafisha maji machafu na kuwapa wananchi maji. Alisema kuwa yeye ni kizazi cha tatu ambao wanafanya kazi ile ya uwekezaji kwa upande wa maji. Nikisema kuwa sekta hii ni mahali watu wanafaa kufungua macho, kuna watu wamefanya kazi hii, vizazi vitatu katika nchi zilizoendelea. Watu wanajua kampuni ile wakiwa ni wao wanatuletea maji miferejini mwetu basi maji yale ni masafi. Hakuna uchafu ndani ya yale maji. Ikiwa ni kampuni ile inasafisha maji, basi yale maji machafu wanaachilia kwa mito yetu na bahari hazitachafua bahari zile kwa sababu wako na uzooefu, ujuzi kwani wamesomea suala hili na kujua namna ya kusimamia biashara ya maji. Bi Spika wa Muda, sheria hii inatangaza mwanzo mpya kwa sekta ya uekezaji wa maji. Wananchi watukufu ambao wanasikiza Seneti inafaa wajipange. Wasipojipanga watapangwa. Kesho utakuwa unasema kuwa kampuni hazifanyi vizuri na ulikuwa unaskiza Bunge la Seneti na hukufanya na mwingine akafanya. Wito wangu ni kuwa wale ambao watasimamia kazi hii ya uewekezaji kati ya Serikali za Kaunti na sisi ambao tutaingia kwa hizi biashara, ya kwamba haki ifanyike. Wale ambao wako na uwezo, haswa wale wako kwenye biashara hii ya kutoa maji na kuuza, na kupeleka kwa water bowsers. Hawa wapewe nafasi za kwanza kufanya ushirika na serikali za kaunti ili wawekeze. Miferiji mipya iwe pale, billing systems mpya ambazo zitakuwa na tokens. Na pia maji yasiwe yanamwagika yakapotea. Ikiwa nimelipia token ya mia mbili basi pesa yangu ifike mia mbili. Kama nimenunua token ya Shilingi elfu moja na ninajua familia yangu, pengine tunatumia maji ya Shilingi elfu moja kwa wiki ama kwa mwezi basi hiyo maji ifike. Tunataka wawekezaji waje kwa sababu sheria tumeitengeneza. Serikali hii ya Kenya Kwanza inajali mambo yetu ambayo inahusika na wananchi. Hili ni jambo nzito kwa wananchi. Shida ya maji ipo na huu ni msingi mwafaka kwa ajili ya mipangilio yetu ya kiserikali. Kwa hivyo, wale ambao wanasikiza Bunge la Seneti wajipange na wajue kuwa Serikali yetu inatujali. Seneti inajali wananchi. Ikiwa watu wataskiza na kufuatilia mswada huu, basi baada ya muda sio mrefu sana tutaanza kupata mabadiliko. Maanake kule kwa gatuzi tutaona hali ikibadilika. Mungu akipenda, sekta hii ya maji ambayo imetusumbua kwa miaka mingi tutaanza kuangalia na mambo yatakuwa mazuri kwa wananchi. Bi. Spika wa Muda, haya yote yako ndani ya Clause 5 ya hii Ripoti ya uwiano kati ya Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti. Nimefurahi sana maelewano ambayo yamekuwa. Kulikuwa na vipengele ambavyo hatukuvikubali sisi hapa Seneti. Tuligeuza na wale wa Bunge la Kitaifa wakakubali. Na kuna vipengele walileta huku hatukuvikubali na tukageuza. Sasa tuko na sheria ambayo iko sawasawa, dhabiti na itasaidia wananchi wetu. Nashukuru kiongozi ambaye alishughulikia Mswada huu Seneta wa Nyandarua. Ameongoza kamati hii pamoja na wabunge wa Bunge la Kitaifa. Tunashukuru kwa kazi mliyofanya ya kuleta uwiano na kujaribu kumaliza utata uliokuwa kwenye vipengele kadha wa kadha. Sasa tuko na sheria mwafaka ambayo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}