GET /api/v0.1/hansard/entries/1490592/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1490592,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1490592/?format=api",
"text_counter": 86,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa kuchangia Hoja hii. Kama Seneta wa Kaunti ya Kwale, kwa niaba ya watu wa Kwale, naunga mkono hii Sugar Bill. Kusema ukweli, kule kwetu kuna matatizo mengi, haswa katika Kiwanda cha Sukari cha Ramisi. Juzi tulikuwa na tatizo lililofanya wafanyikazi wa kiwanda hicho kugoma kwa sababu ya usimamizi mbaya. Wafanyikazi huenda kwa karibu miezi mitano au sita bila mishahara. Bw. Spika, tutakapopitisha huu Mswada, regulations nyingi humu nchini zitaweza kutekelezwa vizuri kwa sababu kuna watu wanaoleta sukari kutoka nchi za nje. Sukari hiyo huagizwa kwa bei rahisi sana na kufanya sukari yetu kukosa soko. Kama walivyosema Sen. Cherarkey na Sen. Sifuna, nawaunga mkono kwa marekebisho yatakayofanyika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}