GET /api/v0.1/hansard/entries/1490851/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1490851,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1490851/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ya kuchangia ripoti ya Kamati ya Uwekezaji wa Umma katika uchunguzi wao wa mashirika ya maji katika kaunti zetu; Mashirika za maji za Amatsi, Bomet, Gusii, Kisumu, Kwale na Nyeri. Maji ni uhai. Inasikitisha kuwa ripoti hii imeweka wazi kuwa kaunti zetu nyingi zina shida ya maji. Mashirika ambayo yamewezeshwa kusimamia maji haya hayajui yanachofanya. Kaunti zetu haziwekezi katika mambo ya maji. Wanataka kampuni zile zilete faida ya kila mwaka lakini hakuna uwekezaji wowote ambao unafanyika. Katika bajeti za kaunti nyingi utapata kwamba mambo ya maji ni zero. Kabla ya kuendelea ningependa kusahihisha Sen. Osotsi aliposema kwamba ile sewage yote ya Mombasa County inaingia katika Bahari ya Hindi pale Kipevu. Sio sehemu ya Kipevu wala ni sehemu ya Changamwe pekee na sio ya Mombasa County nzima. Sehemu zingine hakuna sewage na watu wanatumia yale mashimo ya kawaida. Tulipata kuyafuatilia mambo haya na Sen. Osotsi mwezi wa tano mwaka huu pamoja na kamati yake na ni ya Kipevu. Bw. Spika wa Muda, jambo la kusikitisha ni kuwa mpaka leo hakuja kuwa na maendeleo yoyote pale Kipevu. Vile kulivyokuwa tulipokwenda ndivyo kumebaki kuwa hivyo. Walisema kuwa pesa zitakuwa released na World Bank anytime ili tuweze kumaliza ukarabati uliokuwa unafanyika lakini ni masikitiko kwamba kufikia hadi leo hakuna kazi yoyote ambayo imeendelea pale. Maji ya sewage bado inaingia kwenye Bahari. Bandari ya Mombasa ni ya kimataifa. Hatuwezi kuruhusu sewage iingie katika bandari yetu wakati kuna meli zinakuja, pamoja na mizigo na vyakula. Marekebisho haya yalikuwa ni mradi uliofadhiliwa na World Bank. Tatizo lilikuwa kwamba hawakuweza kuapprove invoice fulani ili waachilie fedha za kutekeleza na kumaliza mradi huo. Bw. Spika wa Muda, hili ni jambo ambalo ningeonmba kamati kama itapata fursa irudi tena ili iangalie kwa makini. Ni aibu kwamba kaunti ya Mombasa inamwaga sewage katika bandari ya Mombasa ambayo ni ya kimataifa. Katika kuangazia mambo yaliyo katika ripoti hii, fedha nyingi zinapotea kwa sababu maji yanapotea bila kuuzwa kwa wananchi ama kwa wale wanayoyahitaji; Kwa kingereza non - revenue water . Miundo msingi ya sehemu nyingi za maji ni pipe ambazo zilijengwa kabla tupate uhuru-1963. Kenya sasa imefika karibu miaka 60 na pipe ni zilezile. Zimejaa kutu ndani na maji yanayobebwa pale haina uhakika wa kwa safi. Wengi wetu siku hizi hatukunywi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}