HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1490852,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1490852/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "maji ya mfereji. Wengi tunakunywa maji ya chupa. Hata hapa katika Bunge hakuna anayekunywa maji ya mrefeji kwa sababu hatuna uhakika kuwa maji yale ni masafi au la. Hasara ya fedha nyingi inapatikana na kampuni hizi kwa sababu miundo msingi ambayo inapeleka maji inapasuka kwa muda mrefu na hakuna anayejua kuwa maji yanamwagika kiholela katika sehemu zile. Kule Mombasa County walianza kutumia smart meters. Lakini zile meters haziwezi kupima maji ambayo haipo. Ikiwa wewe huna maji inayoingia katika tank au nyumba yako basi ukiwekewa ile smart meter hutakuwa umetibu tatizo ambalo liko. Mara nyingi katika uwekezaji wa umuhimu wa mambo ya maji tunafanya kinyume nyume yani our priorities are upside down . Tulikimbilia kuweka smart meters lakini maji katika mifereji hakuna. Kwa hivyo hata kama una smart meter huwezi hesabu kile ambacho hakuna. Bw. Spika wa Muda, tukiangalia maswala ya uekezaji katika kampuni hizi, utapata kwamba ni ule ule mtaji uliwekwa na serikali wakati wa nyuma ndio unatumika kwa zile kampuni. Kampuni nyingi zinapata hasara. Ijapokua kuna haja kubwa ya maji na kila mwananchi anataka kutumia maji, kutoa maji kule yanapatikana mpaka kuyafikisha kwa wanaoyatumia imekua ni shida. Kwa mfano, kule Mombasa, maji yake mengi yanatoka Mzima Springs lakini kutoka wakati ambao hiyo Springs ilijengwa, mwaka ya 1940 mpaka leo, hatujaongeza hata mfereji mmoja. Sisi yetu ni kukarabati mifereji na kuomba pesa za kufanya utafiti jinsi tutajenga mifereji mingine. Leo, ukienda pale Mzima Springs, utasikitika kwamba wale waliweka Mzima Springs, waliweka Mzima I, Mzima II na Mzima III. Lakini, leo baada ya miaka 60 ya uhuru, tuna Mzima I peke yake inayopeleka maji Mombasa. Bw. Spika wa Muda, sehemu nyingine ya maji ya Mombasa ni Mwache Dam na pia inajengwa tena ili isaidie watu wa Mombasa kupata maji rahisi. Lakini, bado kuna mizozo baina ya kaunti zetu. Ijapokua zile sehemu za maji ni za kitaifa, lakini, bado kaunti zetu zina maji. Kwa mfano, hapo nyuma, kulikua na mzozo baina ya Kaunti ya Kwale na Kaunti ya Mombasa kuhusiana na ule mradi wa Mwache. Watu wa kaunti ya Kwale walikua wanasema maji ya Mwache yatumike Kwale peke yake ili hali, yale maji yatapatikana pale Mwache Dam yataweza kutumika Mombasa na kufaidisha watu wa Kwale. Sehemu nyingine inayoleta maji katika kaunti ya Mombasa ni Marere kule Kwale. Hivi majuzi, wale watu wanaokaa zile sehemu za Changamwe na Jomvu kule Mombasa walikosa maji kwa sababu, maji yote ambayo yalitakikana kuja Mombasa, yalipelekwa Kwale mjini ili kusaidia maandalizi ya Mashujaa Day yaliyofanyika juzi. Hayo ni masikitiko makubwa, kwamba tunafungia maji watu karibu milioni moja ili yapelekwe sehemu moja kwa sherehe ya siku moja. Bw. Spika wa Muda, maji ni uhai na hakuna uekezaji wa kibinafsi katika maswala ya maji. Tukiangalia kaunti zetu nyingi, zina water bowser moja ama mbili au zikiwa nyingi, tatu. Mombasa ina nne, moja iko Likoni, Changamwe, Kisauni na Jomvu. Ingekua kaunti zetu zinaekeza katika maswala ya maji, ingekua wananchi wanapata maji ya rahisi na yana uhakika kwa sababu ni masafi na zile kampuni zingepata fedha za kukimu mahitaji yao. Lakini, ukiangalia balance sheet za hizi kampuni, zinaendelea kupata hasara. Inabidi wananchi warudi tena mifukoni yao ili kufadhili hizi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}